Uanzishwaji wa THTU ni matokeo ya kamati za viongozi kutoka matawi ya Vyuo Vikuu vya Umma Tanzania, ambavyo vilifanya kazi kubwa kuanzia mwaka 1998 hadi 2008, lengo likiwa ni kudai maslahi bora, kuunganisha nguvu za pamoja na kuitaka Serikali yetu kuboresha mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania. Kamati za viongozi kutoka Taasisi hizo mwaka 2005 waliunda jopo la pamoja la vyama vya wafanyakazi, vyama vya kitaaluma na mabaraza ya wafanyakazi, kwa nguvu na mshikamano ndiyo iliyopelekea kuundwa kwa kamati ya Rais ya kuangalia matatizo ya wafanyakazi kutoka Taasisi za Elimu ya Juu. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuzaliwa kwa chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU).