NAMNA YA KUWA MWANACHAMA WA THTU (How to be a member)

Wafanyakazi wote wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini wana hiari ya kuwa wanachama wa THTU kama sheria za kazi zinavyolekeza juu ya uhuru wa wafanyakazi kujumuika pamoja kwa hiari.

Register Now
welcome

Masharti ya kuwa mwanachama wa THTU.

  1. Mwanachama wa THTU sharti awe mfanyakazi wa Chuo Kikuu au Chuo Kikuu Kishiriki, Taasisi ya Elimu ya Juu au Taasisi ya Usimamizi wa Elimu ya Juu na awe ni raia wa Tanzania.

  2. Ajaze fomu maalum ya kujiunga na chama cha wafanyakazi kwa mujibu wa sheria.

  3. Maombi ya wanachama wapya yatapelekwa kwenye ofisi ya tawi mahala pa kazi anapofanyia kazi muombaji.

  4. Uongozi wa tawi, bila kuchelewa, utachambua, kufikiria na kuyakubali maombi hayo. Uongozi wa tawi ukiyakataa maombi, utawajibika kutoa sababu za uamuzi huo kwa halmashauri ya tawi.

  5. Tawi litawasilisha Fomu/Taarifa hizo Makao Makuu ya Chama.

Register Now


NAMNA YA KUWA MWANACHAMA WA THTU.

Register Now