Mwanza | 11–12 Septemba 2025
Kamati ya Wanawake ya THTU Taifa imefanya Mkutano wake Mkuu wa 12 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Tukio hili muhimu limewakutanisha viongozi wa Chama, wajumbe kutoka Kamati za Wanawake za Matawi mbalimbali, na wadau wa usawa wa kijinsia kazini.
Cde. Paul Loisulie, Mwenyekiti wa THTU Taifa, alitoa neno la ufunguzi akisisitiza:
“Wanawake ni nguzo ya uongozi wa vyama vya wafanyakazi. Elimu endelevu ni silaha ya mabadiliko.”
Tazama picha za tukio hapa ? https://postimg.cc/gallery/7LtP1NM
"NIA NA MWEKELEO WETU DAIMA NI KUJENGA, TAIFA KWANZA"