TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA YA KATIBU MKUU WA CHAMA


FURSA YA AJIRA

Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) kinatangaza nafasi ya kazi kwa Katibu Mkuu wa Chama.

Hii ni nafasi adhimu kwa kiongozi mwenye maono, uwezo wa usimamizi na ari ya kuwatumikia wafanyakazi wa elimu ya juu nchini.

Unayo sifa, uzoefu na ndoto ya kuleta mabadiliko?
Hii ndiyo nafasi yako ya kuchangia maendeleo ya Chama na Taifa kwa ujumla.

Mwisho wa kutuma maombi: 18 Mei, 2026 saa 6:00 usiku

Tuma maombi yako kupitia: recruitment@thtu.or.tz

“Nia na Mwelekeo wetu daima ni kujenga, Taifa kwanza”

May 4, 2026, 9:59 am